Thursday, August 27, 2015

mashairi ya harmonize aiyola soma hapa (aiyola lyrics by harmonize)


Harmonize - Aiyola

wasafi
aiyo aiyola ieeh
aiyo aiyola aah
mmh
nilifundishwa na bibi kijijini jinsi ya kupenda
na mwanamke hapigwi
na ngumi ila upande wa khanga
tena mapenzi sio ligi nikakubali kushindwa
mi sikufunzwa biradhi
ushindani risasi kwa panga
mbona nilikuthamini
mengi nikakusevia
sikusema hadharani
wengi wakayasikia
sasa umenipanda kichwani
hukumbuki tulipotokea
unaponishusha thamani
kipi nilichokosea
ingawa kidogo nilichopata
nikajinyima uridhike
ila hukujali ukanikatili moyo
majirani walinicheka
ulipoforce nipike
ah sio siri ilinivunja moyo
oh kisirani ugomvi bila chanjo
ni kweli upo moyoni
sina budi nilivue pendo
ingawa kishingo upande

aiyo aiyola ieh
sitoforce unipende
aiyo aiyola ieh
ooh kishingo upande mama
aiyo aiyola ieh
basi bora uendee
aiyo aiyola ieh

sitosema mapenzi basi
nimeumbwa nna moyo
moyo wenye matamanio
na unapenda pia
ila nitaijutia nafsi
nilikufanya chaguo
ah chaguo la moyo
kumbe ulipita njia
ah  ah nilivowanyima ndugu
ni siri nikakutunzia
usijeleta vurugu
akili ukaitibua
najuta kujitia bubu
sitaki vya kusikia
kisa pendo unisulubu
mengi nishayafumbia
mbona nilikuthamini
mengi nikakusevia
sikusema hadharani
wengi wakayasikia
sasa umenipanda kichwani
hukumbuki tulipotokea
unaponishusha thamani
kipi nilichokosea
oh kisirani ugomvi bila chanjo
ni kweli upo moyoni
sina budi nilivue pendo
ingawa kishingo upande
aiyo aiyola ieh
sitoforce unipende
aiyo aiyola ieh
ooh kishingo upande mama
aiyo aiyola ieh
basi bora uendee
aiyo aiyola ieh

ingawa kishingo upande
aiyo aiyola ieh
sitoforce unipende
aiyo aiyola ieh
ooh kishingo upande mama
aiyo aiyola ieh
basi bora uendee
aiyo aiyola ieh
kishingo upande x2
aaaaah


Image result for harmonize aiyola






4 comments: