Kwa kutumia njia za kisayansi unaweza yafanya maji machafu yawe salama kwa matumizi yako nyumbani, kwa nchi ambazo wananchi wake wana tabu ya maji, au kuna tatizo la upatikanaji wa maji safi kama Tanzania. Unaweza tumia njia hii nyumbani kwako kupata maji safi.
Yafuatayo ni maelekezo ya kuyafanya maji yako yawe safi na salama
1. Chukua kopo la maji ya kunywa, chenye ujazo wa lita moja na kuendelea
2. toboa matundu kadhaa kwenye kifuniko cha kopo
3.kata upande wa chini wa kopo, kuondoa kitako chake
4. andaa mchanga ulio safi, kokoto za saizi ndogo sana (kubwa kidogo kwa mchanga), karatasi laini (tissue), na mkaa kiasi cha gram 150 mpaka 250
4. funga kopo lako kwa kifuniko ulichokitoboa
5.weka kiasi kidogo cha tissue (karatasi laini) moja au mbili ndani ya kopo
6.weka mchanga ulio safi ndani ya kopo baada ya tissue
7. weka mkaa uwe wenye saizi ndogo (chenga)
8. weka kokoto zenye saizi kama ilivoelekezwa hapo juu
9. weka tena karatasi laini (tissue moja au mbili (ikae katika mtido wa kutengeneza shimo ili maji yachujwe kipindi yanaingia kwenye kopo
10. mimina taratibu maji yako ambayo ni machafu wakati ukiwa umekinga chombo cha kupokelea maji yalochujwa upande wa chini
11. maji yako sasa ni safi, sasa waweza tumia njia nyingine za kutibu naji ili yawe salama, kama kutumia chlorine, kuchemsha na nyinginezo zinazoshauriwa kitaalamu.
WAWEZA ANGALIA PIA VIDEO HII HAPA CHINI IKIONESHA HIZO HATUA
0 comments:
Post a Comment