Sunday, September 13, 2015

wanafunzi wa shule ya sekondari Ngudu wafurahia huduma ya maji ya bomba


 
hali ilivyokua kabla ya huduma ya maji kusogezwa karibu 

Shule ya Ngudu iliyopo wilayani kwimba ni moja ya shule iliyokumbana na tatizo la ukosefu wa walimu, pamoja na wanafunzi wake kukosa vipindi kwa muda mrefu kwa tatizo la ukosefu wa maji.
Kwa mujibu wa mhandisi wa maji wa wilaya hiyo Boaz Pius http://www.worldbank.org watu walikua wakipata maji ya bomba kwa masaa matatu mpaka manne kwa siku na wakati mwingine kutopata kabisa, walikuwa wakitegemea maji ya visima sita vilivyochimbwa na waingereza miaka ya 1950.
lakini kwa sasa serikali kwa msaada wa world bank wameweza kuwaletea maji ya bomba eneo hilo.
huduma hiyo imesaidia kwani mwanzo hata watoto wa shule ya sekondari Ngudu na walimu walilazimika kukatisha vipindi kutokana na ukosefu huo wa maji laini kwa sasa hawapati usumbufu huo tena.
wananchi wa eneo hilo wameufurahia mradi huo ulioanza kwa idadi ya makazi yapatayo 700 kuunganishwa na huduma hiyo ya maji,
kupitia mradi wa kahama shinyanga water supply authority KASHYWASA.
 
HALI ILIVO SASA

0 comments:

Post a Comment