Sunday, September 20, 2015

kwanini glass huweza kupasuka ikiwekewa maji ya moto (WHY DOES GLASS BREAK WHEN POURED WITH HOT WATER)

glass huweza kupasuka ikiwekewa kimiminika cha moto kwa sababu kuu moja, glass inapowekewa kitu cha moto, mabadiliko hayo ya jotoridi hupokelewa na upande wa ndani wa glass, joto hilo husababisha upande huo wa glass kutanuka, endapo upande wa nje wa glass utatanuka kwa uwiano wenye tofauti kubwa na ule wa ndani basi nyufa huweza kutokea kwenye glass hiyo, na hatimaye kupasuka kabisa.
Vivyo hivyo maji ya baridi sana huweza kupasua glass endapo mabadiliko ya jotoridi la ndani ya glass yatatofautiana na ya nje kwa uwiano mkubwa, yaani kusinyaa kwa glass upande wa ndani utatofautiana sana na upande wa nje.

NINI KIFANYIKE KUZUIA HI
1. Mimina maji au kimiminika chako taratibu ili kuifanya glass iendane na jotoridi la kiminika hicho, hii itasaidia kuepukana na tatizo la kupasuka kwa glass yako
2. Pia kwa kimiminika cha moto glass yaweza kupashwa moto kwa kuiweka sehemu yenye digrii 40-50 za jotoridi

UNAWEZA JIFUNZA KITU KINGINE PIA HAPO
Hata katika maisha ya kawaida ya binadamu, kupokea mabadiliko yoyote, ni lazima uwe umejiandaa kuyapokea, na mabadiliko yoyote yale kwa mtu yanaanzia kwake, yaani moyoni mwake, ukiwa tayari kubadilika wewe ndipo mtu mwingine anaweza kukuletea mabadiliko.
CHANGE NI WEWE.

Thursday, September 17, 2015

majina ya waliokosa vyuo (wanaotakiwa kuomba kwa mara nyingine 2015?2016)

Click link hii kuangalia majina ya wanaotakiwa kuomba kwa mara nyingine kujiunga na vyuo vikuu 2015/2016. Hii ni baada ya kukosa nafasi katika maombi yao ya kwanza.
 Kwa herufi kati ya A-H
http://www.tcu.go.tz/images/pdf/Group%20(A_H).pdf
  Kwa herufi kati ya I-L
http://www.tcu.go.tz/images/pdf/Group%20(I_L).pdf
 Kwa herufi kati ya M-N
http://www.tcu.go.tz/images/pdf/Group%20(M_N).pdf
 Kwa herufi kati ya O-Z
http://www.tcu.go.tz/images/pdf/Gruop%20(O_Z).pdf

Sunday, September 13, 2015

wanafunzi wa shule ya sekondari Ngudu wafurahia huduma ya maji ya bomba


 
hali ilivyokua kabla ya huduma ya maji kusogezwa karibu 

Shule ya Ngudu iliyopo wilayani kwimba ni moja ya shule iliyokumbana na tatizo la ukosefu wa walimu, pamoja na wanafunzi wake kukosa vipindi kwa muda mrefu kwa tatizo la ukosefu wa maji.
Kwa mujibu wa mhandisi wa maji wa wilaya hiyo Boaz Pius http://www.worldbank.org watu walikua wakipata maji ya bomba kwa masaa matatu mpaka manne kwa siku na wakati mwingine kutopata kabisa, walikuwa wakitegemea maji ya visima sita vilivyochimbwa na waingereza miaka ya 1950.
lakini kwa sasa serikali kwa msaada wa world bank wameweza kuwaletea maji ya bomba eneo hilo.
huduma hiyo imesaidia kwani mwanzo hata watoto wa shule ya sekondari Ngudu na walimu walilazimika kukatisha vipindi kutokana na ukosefu huo wa maji laini kwa sasa hawapati usumbufu huo tena.
wananchi wa eneo hilo wameufurahia mradi huo ulioanza kwa idadi ya makazi yapatayo 700 kuunganishwa na huduma hiyo ya maji,
kupitia mradi wa kahama shinyanga water supply authority KASHYWASA.
 
HALI ILIVO SASA

Sunday, September 6, 2015

tambua jinsi ya kuyafanya maji machafu yawe safi na salama kwa matumizi ya nyumbani na hata kunywa

Kwa kutumia njia za kisayansi unaweza yafanya maji machafu yawe salama kwa matumizi yako nyumbani, kwa nchi ambazo wananchi wake wana tabu ya maji, au kuna tatizo la upatikanaji wa maji safi kama Tanzania. Unaweza tumia njia hii nyumbani kwako kupata maji safi.

 Image result for tatizo la maji afrika

 Yafuatayo ni maelekezo ya kuyafanya maji yako yawe safi na salama
1. Chukua kopo la maji ya kunywa, chenye ujazo wa lita moja na kuendelea
2. toboa matundu kadhaa kwenye kifuniko cha kopo
3.kata upande wa chini wa kopo, kuondoa kitako chake
4. andaa mchanga ulio safi, kokoto za saizi ndogo sana (kubwa kidogo kwa mchanga), karatasi laini (tissue), na mkaa kiasi cha gram 150 mpaka 250
4. funga kopo lako kwa kifuniko ulichokitoboa
5.weka kiasi kidogo cha tissue (karatasi laini) moja au mbili ndani ya kopo
6.weka mchanga ulio safi ndani ya kopo baada ya tissue
7. weka mkaa uwe wenye saizi ndogo (chenga)
8. weka kokoto zenye saizi kama ilivoelekezwa hapo juu
9. weka tena karatasi laini (tissue moja au mbili (ikae katika mtido wa kutengeneza shimo ili maji yachujwe kipindi yanaingia kwenye kopo
10. mimina taratibu maji yako ambayo ni machafu wakati ukiwa umekinga chombo cha kupokelea maji yalochujwa upande wa chini
11. maji yako sasa ni safi, sasa waweza tumia njia nyingine za kutibu naji ili yawe salama, kama kutumia chlorine, kuchemsha na nyinginezo zinazoshauriwa kitaalamu.
WAWEZA ANGALIA PIA VIDEO HII HAPA CHINI IKIONESHA HIZO HATUA


Saturday, September 5, 2015

mara nyingi mashabiki wa muziki huendana na tabia zao isome hapa

 mwaka 2008 utafiti uliofanywa kwa watu zaidi ya 36000 kutoka duniani kote ulihitimisha kuwa ladha ya muziki na aina ya maisha wanayoishi mashabiki wake vina uhusiano mkubwa.Utafiti ambao ulifanywa na Profesa Adrian kutoka chuo kikuu cha Heriot Watt Kaskazini, Edinburgh ulionesha kuwa
Mashabiki wa muziki "classic" walikua ni wenye aibu, wakati mashabiki wa muziki unaotumia vyombo vizito kama rock walikuwa ni wapole na wenye furaha. Mashabiki wa muziki wa kiindi si wenye kujithamini sana, na wasio na bidii, mashabiki wa muziki wa rap ni wenye kujithamini sana na wenye kwenda na wakati, mashsbiki wa muziki wa country na R&B ni wenye bidii,na wenye kwenda na wakati, mashabiki wa muziki wa muziki wa reggae ni wabunifu nawasio na bidii, mashabiki wa pop ni wenye kujithamini, si wabunifu lakini wenye bidii na wenye kwenda na wakati.

 2008, A study of more than 36,000 people from around the world concluded that musical tastes and personality type were closely related. The research, which was carried out by Professor Adrian North of Heriot Watt University, Edinburgh in the UK suggested classical music fans were shy, while heavy metal fans were gentle and at ease with themselves. Fans of Indie music had low self-esteem and were not hard working, fans of Rap music had high self-esteem and were outgoing. Country & Western fans were hardworking and outgoing, Reggae fans were creative but not hardworking, and fans of chart pop had high self-esteem, were not creative, but where hardworking and outgoing.

Thursday, September 3, 2015

mashairi ya wimbo nice couple kutoka kwa mayunga (nice couple lyrics by mayunga)

Mayunga - nice couple

intro

by show by show
by show oooh by show
by show by show
by show oooh baby by show

verse I
by show i love you baby
to the baby to the sir
aisee umepanda grade
na ni mzuri si utani
sikuachi waniue may be
nikukose maishani
penzi letu uzito wa tani
halipimwi kwa mizani eeh

bridge
aiya iya iyaaa
iyelele mama ooh iye iye
aiya iya iya iya (njoo tudance aah)
aiya iya iyaaa
iyelele mama ooh iye iye
aiya iya iya iya (ngororo tokobina ayaya)
chorus
mi na wewe nice couple (mi na wewe nice couple)
mi na wewe double double (njoo tudance hakuna kokoro)
mi na wewe nice couple (mi na wewe nice couple)
mi na wewe double double (ale tokobina hakuna kokoro)
ale nice nai eeh
nice hakuna kokoro
ale nice nai eeh
nice hakuna kokoro
ooh ooh aah
hakuna kokoro
Image result for mayunga
parare parare
 pararee parare

verse II

looking at my beatiful baby
she knows how to shake body
ukitaka cheza naye
lazima kwanza unione
tena ujue kucheza
parare parare
ujue kuzungusha
parare parare
aah to the left
parare parare
oh to the right
parare parare
ooh nananananaaa
oh nananannaaa
ukiwa nami jiamini
wasiwasi uwe pembeni
wanasema ya chinichini hawayaji ya ndani
wana wivu kama nini
tabia za kishitwani
wanasubiri gizani
sisi tuko nuruni

bridge

aiya iya iyaaa
iyelele mama ooh iye iye
aiya iya iya iya (ngororo njoo tudance aah)
aiya iya iyaaa
iyelele mama ooh iye iye
aiya iya iya iya (ngororo tokobina ayaya)
chorus
mi na wewe nice couple (mi na wewe nice couple)
mi na wewe double double (njoo tudance hakuna kokoro)
mi na wewe nice couple (mi na wewe nice couple)
mi na wewe double double (ale tokobina hakuna kokoro)
ale nice nai eeh
nice hakuna kokoro
ale nice nai eeh
nice hakuna kokoro
ooh ooh aah
hakuna kokoro

outro
parare parare
 parare parare
parare parare
 pararee parare
oooh nananananaa
oh nananaaaa